Saturday, February 7, 2009

NAKUPENDA TU - DUDU BAYA

Friday, February 6, 2009

MTOTO AKILILIA WEMBE - MLIMANI PARK ORCHESTRA



Mtoto akililia wembe wacha umkate
Ata(ka)popata kidonda ndipo ata(ka)pouogopa
Dada yetu wewe, ulikwishaolewa
Lakini kwa tama yako
Ulikubali kuacha watoto wako
Ukaivuruga na ndoa yako
Kwenda kuishi na bwana mwingine eee
Vimekukuta vya kukukuta
Mwenyewe umetutangazia
Majuto ni mjukuu
Tukusaidie nini sema
Nduguzo tulikuasa na mapema
Kwamba bwana huyo mdanganyifu
Hodari sana wa kuoa na kuacha
Ukatuona sisi watu fitina
Tunakuonea gere
Umepata bwana mwenye pesa eee


Atakujengea nyumba
Atakununulia gari eee
Sasa unajuta


Usilie eee
Usilie dada
Unalia nini
Nawe ulisema
Umempata bwana
Atakayekufaa maishani mwako
Halooo dada
Halooo “sister



Sisi tulijua
Nyumba hiyo ni chambo tu
Si(y)o kwako peke yako dada eee
Hata hao walioolewa kabla yako wakaachika
Tunawaona mitaani kila siku
Tunapanda nao UDA na daladala eee
Hakuna cha gari wala kibanda walichoambulia
Pole dada uliyataka mwenyewe

Usilie eee
Usilie dada
Unalia nini
Nawe ulisema
Umempata bwana
Atakayekufaa maishani mwako
Halooo dada
Halooo “sister”



CINDERELLA - ALI KIBA

MUME BWEGE - BUSHOKE














Nilikuwa na mpenzi wangu

Nani asiyemjua

Mtoto kaumbika

Utasema malaika

Miezi kadhaa ikasogea

Mtoto (wa) kwanza tukazaa

Mtoto katoka Mwarabu

Swali lilikosa jibu

Akasema we hujui

Mtoto kafata kwa babu

Nikagunaguna pale mzee nikauchuna


Mtoto (wa) pili tukazaa

Huyu wa sasa Mchina doh

Nikasema mama vipi

Mbona mi sielewi

Akasema we hujui

Huyu kafata kwa bibi


Aa wewe mama wee

Ingekuwa ungefanyeje


Mwenzenu nalala chini

Mke wangu kitandani

Nikilala kitandani

Kila mtu shuka lake

Mwenzenu nalala chini

Mke wangu kitandani

Nikilala kitandani

Basi ujue mzungu wa nne


Nikiuliza kwa nini

Anasema amenipa likizo eeh

Siyo kama napenda

Imenilazimu ooh

Siyo kama napenda

Ananilazimisha yoo


Mwenzenu naosha vyombo

Mwenzenu napiga deki

Mzee mzima napika

Jamani nafua nguo

Siyo kama napenda

Nalazimishwa mimi


Lo, hii sasa kali

Jana kaniambia anataka kwenda klabu na marafiki zake

Ila kaniambia mimi

Nilinde nyumba eti wezi wasije wakaiba

Eee Bize Man hii halali kweli

Oyaa Mbiye njoo unisaidie huku nyumbani mwenziyo naonewa

Chifu Rumanyika, unajifanya hujui

Ooo naonewa mimi

Aa wewe mama wee

Ingekuwa ungefanyeje


MSAMIATI


-jua - fahamu

umbika - naturally attractive

mzungu wa nne - opposite direction

likizo - mapumziko

lazimu - ni lazima

lazimisha - force to do something

osha - wash

vyombo - dishes

piga deki - kusafisha sakafu

fua nguo - wash clothes

linda - protect

wezi - wingi wa mwizi

iba - steal

halali - fair

onea - mistreat